Explore Swahili Poems (Mashairi)

Penzi Kibarua

by JackSwaleh

Nakukosea kwa kweli, nimekosa kutimiza
Ni ile ile tu hali, ya kesho yabaki giza
Sijui cha kubadili, nashinda nikikuwaza
Naanza kujikubali, kuwa nawe sitaweza

Ajira nimeshikika, bosi hatuelewani
Muda hata wa kupoka, naukosa...

Lawamu Za Sababu

by JackSwaleh

Sababu za sababu hizi nini
Sababu yako haswa ni nini
Lawama, ni nani wa kulaumu
Lawama na sababu zitaisha lini
Kama si sababu ni lawama
Basi ni sababu za lawama
Lawama za sababu hadi lini

Naamini Nitafika

by JackSwaleh

Nyimbo zangu barabara, kwa lugha ya Kiswahili
Viwango vya maabara, utunzi haujafeli
Mbinu yangu sijapora, jua akili ni mali
Kila siku nitachora, ubunifu hu ni ghali

Nipe kalamu mi bubu, nataka kusemezana
Makini na taratibu,...

Ndoa Ndoano

by Kakakizzy

Ndoa jamani ndoano, mwanamwali sikimbie
Nimeshaona watano, si usemi msikie
Kuigaiga mifano, mbio mbovu mtulie
Mambo mazuri rafiki, upesi si mwendo wake

Ndoa jamani ndoano, ilo na chambo pembeni
Yavutia kwa maono, ushoboke...

Natamani

by Kakakizzy

Siku nyingi natamani, udurusu ya moyoni
Hino zito ya uzani, niitoe mtimani
Ujuwe sina utani, ninapokuita hani
Siku niloitamani, leo dhahiri machoni

Jamani ninatamani, moyo ngekua kitabu
Ungefungua zamani, ewe waangu...

Nilipotoka ni Mbali

by JackSwaleh

Nilipotoka ni mbali, kesho nayo majaliwa
Namshukuru Jalali, maisha kanipa mbawa
Kanilinda zote hali, kwangu tamu tu mliwa
Hapa ni kwangu manzili, mie nimebarikiwa

Raha ninayo moyoni, fikira nazo tulivu
Wa pili shajua nani,...

Jumapili

by Kakakizzy

Mola Rabuka Manani, Mungu Mterehemezi
Leo twaja kwa imani, twazileta kwa Mwenyezi
Dua zetu za moyoni, Japo hatukupendezi
Ridhia kutujalia, yale tunayoombea