This is JackSwaleh

author image

Kiswahili lugha bahari
Mashua yangu mashahiri
Niongeze umahiri
Karibuni tukariri

JackSwaleh™

My recent content

Penzi Kibarua

by JackSwaleh

Nakukosea kwa kweli, nimekosa kutimiza
Ni ile ile tu hali, ya kesho yabaki giza
Sijui cha kubadili, nashinda nikikuwaza
Naanza kujikubali, kuwa nawe sitaweza

Ajira nimeshikika, bosi hatuelewani
Muda hata wa kupoka, naukosa...

Hali Gani Hii Ghali

by JackSwaleh

Moyo wangu wasumbuka, yaganda ya kwangu damu
Nafsi yasononeka, hali kwani yahujumu
Mwenzenu nadhoofika, maisha yanidhulumu
Hadi lini kufinyika, tayari nishagharimu

Adimu hizi mihela, majukumu yazidia
Hamuna hata cha kula,...

Lawamu Za Sababu

by JackSwaleh

Sababu za sababu hizi nini
Sababu yako haswa ni nini
Lawama, ni nani wa kulaumu
Lawama na sababu zitaisha lini
Kama si sababu ni lawama
Basi ni sababu za lawama
Lawama za sababu hadi lini

Mawazo Waziwazi

by JackSwaleh

Ninayowaza siwezi eleza
Kueleza natatizika
Natatizika na haya mawazo
Mawazo kuyawazua yawe wazi
Nayawazia tena sana
Ninayowaza siwezi eleza

Uanadamu Adimu

by JackSwaleh

Ni kweli wakati wote nakaa mwenye hasira
Ni kweli kabisa sura yangu imekunjika
Ukinitazama ni kama sina furaha yoyote
ni kama sina fani kwa lolote
Ni kweli nimesononeka
Ni kweli haya yote
Maisha yangu yote nimekuwa...

Angalau Rudi Baba

by JackSwaleh

Angalau rudi baba, tusemezane kwaheri
Mchungu sana hu mwiba, hadi naumwa sadiri
Tumepatwa na msiba, ni nani katusihiri
Simanzi limetukaba, kifo kimekusairi

Sote tumekuwa bubu, sauti zimetutoka
Hii nayo ni sulubu, chozi...

Baba Wetu wa Mbinguni

by JackSwaleh

Baba wetu wa mbinguni, mbele zako nimerudi
Niko chini magotini, hali yangu inabidi
Kwa kukosoa imani, mema nikayakaidi
Nimepoteza ramani, pole kwa kubaidi

Yule mwovu kaninasa, kanipa vya ulimwengu
Kapiga zote anasa,...

Ipo Siku Naamini

by JackSwaleh

Ipo siku naamini, ya kwangu yatabadili
Yatanitoka moyoni, iwe bora tena hali
Utulivu akilini, isizame yangu meli
Nikapate tu amani, dua langu kwa Jalali

Ipo siku ndugu yangu, utatabasamu tena
Yataisha tu machungu, shida...

Kuwa Nawe ni Ajali

by JackSwaleh

Yangu rununu hushiki, ujumbe sipati hata
Labda sijawafiki, usingehofu kusuta
Waona siwajibiki, kuelezwa sitakata
Hali sasa taharuki, mimi sitaki kujuta

Moyo wangu nilikupa, penzi lako nikazama
Nikakupenda kwa pupa, ukawa we...

Kwaheri ya Kuonana

by JackSwaleh

Najawa na wasiwasi, sina kamwe utulivu
Moyo wapiga kwa kasi, zapungua zangu nguvu
Navunjika kwa wepesi, nakubali mi potovu
Taabu zinenikisi, nakaribia majivu

Mbona mie nasulubu, na jihisi takataka
Kuishi sina sababu, msukumo...

Mjini Kimeumana

by JackSwaleh

Mjini kimeumana, nazidiwa maarifa
Mazito yananibana, zinaongezeka nyufa
Najaribu kukazana, marefu sana masafa
Ndoto zabakia dhana, mkweche nango ja mafa

Maisha huku magumu, heri kule kijijini
Najificha mumu humu, nazidiwa na...

Moyo Wangu Wasumbuka

by JackSwaleh

Moyo wangu wasumbuka, yaganda ya kwangu damu
Nafsi yasononeka, hali kwani yahujumu
Mwenzenu nadhoofika, maisha yanidhulumu
Hadi lini kufinyika, tayari nishagharimu

Adimu hizi mihela, majukumu yazidia
Hamuna hata cha kula,...

Moyo Wangu Waugua

by JackSwaleh

Moyo wangu waugua, nasononeka kwa ndani
Nguvu zinanipungua, yaniishia imani
Laiti ningali jua, kiburi changu kiini
Nayo nishaichemua, mbelezo narudi chini

Tangu ulipoondoka, ni kweli kimeniramba
Mwenzio nahangaika, jinsi...

Naamini Nitafika

by JackSwaleh

Nyimbo zangu barabara, kwa lugha ya Kiswahili
Viwango vya maabara, utunzi haujafeli
Mbinu yangu sijapora, jua akili ni mali
Kila siku nitachora, ubunifu hu ni ghali

Nipe kalamu mi bubu, nataka kusemezana
Makini na taratibu,...

Nilipotoka ni Mbali

by JackSwaleh

Nilipotoka ni mbali, kesho nayo majaliwa
Namshukuru Jalali, maisha kanipa mbawa
Kanilinda zote hali, kwangu tamu tu mliwa
Hapa ni kwangu manzili, mie nimebarikiwa

Raha ninayo moyoni, fikira nazo tulivu
Wa pili shajua nani,...

Niwacheni Tu Jamani

by JackSwaleh

Niwacheni tu jamani, hamuwezi nielewa
Zimezidi zenu shani, semi zenu zaniwawa
Mwang'ata kama kunguni, mwaumiza kama chawa
Haya yangu madhumuni, najua sijachelewa

Mzaha sasa usaha, mie munanihujumu
Raha sasa karaha, kamwe...

Subira Yaniumiza

by JackSwaleh

Subira yaniumiza, yatakuwa sawa lini
Hali kweli imekaza, nachotaka sikioni
Jasho bure kupanguza, nasubiriyo laini
Nguvuzo nitajijaza, kujikaza kisabuni

Maisha tu kuinama, nikiinuka bahati
Mjini na jituma, kijijini...

Tamu Imekuwa Chungu

by JackSwaleh

Tamu imekuwa chungu, raha geuka karaha
Nalilia nchi yangu, yadhorora yake siha
Kenya kipenzi chungu, nafata gani nasaha
Lavunjika hili jungu, tunaipoteza njia

Kosa gani tunatenda, vijana kujieleza
Raisi tunakupenda, sauti...

Usiku Bila Nuru

by JackSwaleh

Usiku bila nuru, kimya kote katanda
Kichwa mawazo nduru, hakuna lepe kitanda
Njia zote fungika, tayari fika mwisho
Gumu hili labaka, Mola nipangie kesho

Ngumu swali kujibu, kuelewa hali yangu
Sezi mimi bubu, kueleza soni...

Vuta Nikuvute Tena

by JackSwaleh

Vuta nikuvute tena, mwenzanguwe kulikoni
Maneno mengi wachana, wewe huna hata soni
Yalibakia ya jana, sababuyo siioni
Huchoki kukimbizana, kwani kageuka jini

Usinitie kiwewe, wachana nami kabisa
Usitupe kwangu mawe, iwe ni...

We mnyang'anyi jameni

by JackSwaleh

We mnyang'anyi jameni, sasa mbona hivi kweli
Nasema nawe mhuni, waona hii halali?
Nimechumia juani, usiku pia silali
Sasa hapo kivulini, wakula ya kwangu mali

Wazunguka na kiburi, kwangu chungu na machozi.
Mjini sasa ni...

Zangu Zifike Salamu

by JackSwaleh

Zangu zifike salamu, nangoja yako jawabu
Bado niko mumu humu, kaniachia taabu
Najikaza nasaumu, rudi naomba jaribu
Niambie utakamu, gonjwa hili ulitibu

Hukunipa mi ilani, hata ya mwisho kwaheri
Ulienda pande gani, pekee...

Kelele Kengele

by JackSwaleh

Ni nyingi kelele akilini
Napotulia, akili mna kelele
Nitalia hadi lini — ninazidiwa
Napojaribu kutulia, kengele zaongezeka
Ama natokwa na wazimu mimi
Naona ni kama sijielewi
Ni nyingi kelele akilini

Hayawi Hayawi Huwa

by JackSwaleh

Hayawi hayawi huwa
Ukiona vyaelea jua vimeundwa
Kama halipo basi laja
Linalokusudi lina kusudi
Chunga usiwe mpango au mpangoni
Unayoyaona ni hivyo tu
Ajuaye pekee Maulana
Binadamu hugeuka

Mpungufu Binadamu

by JackSwaleh

Mpungufu binadamu, yeyote kiasi chake
Kuwa kamili adimu, kila mja na makeke
Yeyote yamugharimu, kuficha ubaya wake
Ni hujuma kulaumu, ati sema ikutoke

Kunena siwe mwepesi, legeza za kwako ndewe
Waelewe adinasi, usipo waache...