Explore Swahili Poems (Mashairi)

Niwacheni tu jamani, hamuwezi nielewa
Zimezidi zenu shani, semi zenu zaniwawa
Mwang'ata kama kunguni, mwaumiza kama chawa
Haya yangu madhumuni, najua sijachelewa
Mzaha sasa usaha, mie munanihujumu
Raha sasa karaha, kamwe...

Nyimbo zangu barabara, kwa lugha ya Kiswahili
Viwango vya maabara, utunzi haujafeli
Mbinu yangu sijapora, jua akili ni mali
Kila siku nitachora, ubunifu hu ni ghali
Nipe kalamu mi bubu, nataka kusemezana
Makini na taratibu,...

Yangu rununu hushiki, ujumbe sipati hata
Labda sijawafiki, usingehofu kusuta
Waona siwajibiki, kuelezwa sitakata
Hali sasa taharuki, mimi sitaki kujuta
Moyo wangu nilikupa, penzi lako nikazama
Nikakupenda kwa pupa, ukawa we...

Moyo wangu wasumbuka, yaganda ya kwangu damu
Nafsi yasononeka, hali kwani yahujumu
Mwenzenu nadhoofika, maisha yanidhulumu
Hadi lini kufinyika, tayari nishagharimu
Adimu hizi mihela, majukumu yazidia
Hamuna hata cha kula,...

Uzuri wake waridi🌹, likupendeze machoni
Kwenye upepo baridi, harufu nzuri puani
Litimie ja ahadi, likaote mtimani
Mie mvua samaki, kwako nimevua lulu

Mola Rabuka Manani, Mungu Mterehemezi
Leo twaja kwa imani, twazileta kwa Mwenyezi
Dua zetu za moyoni, Japo hatukupendezi
Ridhia kutujalia, yale tunayoombea

Nakukosea kwa kweli, nimekosa kutimiza
Ni ile ile tu hali, ya kesho yabaki giza
Sijui cha kubadili, nashinda nikikuwaza
Naanza kujikubali, kuwa nawe sitaweza
Ajira nimeshikika, bosi hatuelewani
Muda hata wa kupoka, naukosa...

Ni nyingi kelele akilini
Napotulia, akili mna kelele
Nitalia hadi lini — ninazidiwa
Napojaribu kutulia, kengele zaongezeka
Ama natokwa na wazimu mimi
Naona ni kama sijielewi
Ni nyingi kelele akilini

Siku nyingi natamani, udurusu ya moyoni
Hino zito ya uzani, niitoe mtimani
Ujuwe sina utani, ninapokuita hani
Siku niloitamani, leo dhahiri machoni
Jamani ninatamani, moyo ngekua kitabu
Ungefungua zamani, ewe waangu...

Ndoa jamani ndoano, mwanamwali sikimbie
Nimeshaona watano, si usemi msikie
Kuigaiga mifano, mbio mbovu mtulie
Mambo mazuri rafiki, upesi si mwendo wake
Ndoa jamani ndoano, ilo na chambo pembeni
Yavutia kwa maono, ushoboke...

Mjini kimeumana, nazidiwa maarifa
Mazito yananibana, zinaongezeka nyufa
Najaribu kukazana, marefu sana masafa
Ndoto zabakia dhana, mkweche nango ja mafa
Maisha huku magumu, heri kule kijijini
Najificha mumu humu, nazidiwa na...

Ninayowaza siwezi eleza
Kueleza natatizika
Natatizika na haya mawazo
Mawazo kuyawazua yawe wazi
Nayawazia tena sana
Ninayowaza siwezi eleza