Vuta nikuvute tena, mwenzanguwe kulikoni
Maneno mengi wachana, wewe huna hata soni
Yalibakia ya jana, sababuyo siioni
Huchoki kukimbizana, kwani kageuka jini
Usinitie kiwewe, wachana nami kabisa
Usitupe kwangu mawe, iwe ni yangu makosa
Waniwinda sana mwewe, taabani wajitosa
Hebu niachie wewe, isije iwe mkasa
Sibishane nami tembo, utapasuka msamba
Mkizi hasira nembo, mwishowe gonga tu mwamba
Nilvuka niko ng'ambo, huning'ati ng'o we mamba
Achanayo haya mambo, shingo wa jitia kamba