Usiku bila nuru, kimya kote katanda
Kichwa mawazo nduru, hakuna lepe kitanda
Njia zote fungika, tayari fika mwisho
Gumu hili labaka, Mola nipangie kesho
Ngumu swali kujibu, kuelewa hali yangu
Sezi mimi bubu, kueleza soni kwangu
Topeni mi shazama, isha tumbukia nyongo
Alia sana mama, kaniona mimi muongo
Siku zote tamani, mazuri mema maisha
Ona sina sinani, akiba nayo kwisha
Ajira sijapata, serikali kadanganya
Kuishi ni matata, angalau muza nyanya