Ni kweli wakati wote nakaa mwenye hasira
Ni kweli kabisa sura yangu imekunjika
Ukinitazama ni kama sina furaha yoyote
ni kama sina fani kwa lolote
Ni kweli nimesononeka
Ni kweli haya yote
Maisha yangu yote nimekuwa vitani
Mwili waniwawa kwelikweli
Moyo wangu umejawa majeraha tele
Nimekosa kamwe mawazo tulivu
Hali yangu imekuwa duni
Wa kueleza nimekosa,
simuamini yeyote yule kwa kuwa walonipiga ni wawa hawa binadamu
Nimelowa majonzi na huruma kwa wingi
Naogopa kubaki pekee kwa hofu ya kujidhuru
Kinaya ni kuwa kwa sasa si eti nina hasira
Hamu ya kutaka kuwa na furaha yanifanya nikae mwenye mori
Kuwa mwenye bashasha ni vita vingine ambavyo najizatiti kushinda,
zaidi ya kunifanya niwe hayawani
Hilo ndani langu ni vita tosha!
Uanadamu Adimu
by JackSwaleh , August 8, 2024
Unaeza penda kusoma: "Ndoa Ndoano"