Subira yaniumiza, yatakuwa sawa lini
Hali kweli imekaza, nachotaka sikioni
Jasho bure kupanguza, nasubiriyo laini
Nguvuzo nitajijaza, kujikaza kisabuni
Maisha tu kuinama, nikiinuka bahati
Mjini na jituma, kijijini nidhibiti
Kila siku kujipima, isiwe ninakaputi
Kalamu wino watema, Mungu ingilia kati
Dua langu kwa Mwenyezi, hali yangu kubadili
Ingawa njia telezi, magumu nayakabili
Haziishi pingamizi, kamwe ninazike jeli
Kugona mie siwezi, kupigana nakubali