Siku nyingi natamani, udurusu ya moyoni
Hino zito ya uzani, niitoe mtimani
Ujuwe sina utani, ninapokuita hani
Siku niloitamani, leo dhahiri machoni
Jamani ninatamani, moyo ngekua kitabu
Ungefungua zamani, ewe waangu muhibu
Mwanzo hadi ukingoni, kurasa zote swahibu
Nitoke changamotoni, kueleza ni sulubu