Naamini Nitafika

by JackSwaleh , August 15, 2024

Nyimbo zangu barabara, kwa lugha ya Kiswahili
Viwango vya maabara, utunzi haujafeli
Mbinu yangu sijapora, jua akili ni mali
Kila siku nitachora, ubunifu hu ni ghali

Nipe kalamu mi bubu, nataka kusemezana
Makini na taratibu, busara nitamimina
Polepole niwe kubu, nitazidi kukazana
Siku zote nitasubu, kazi yangu iwe sena

Mahali pema peponi, Walibora pumzika
Nazidi kuwa makini, kama we niwe tajika
Nadhukuru kwa ramani, tayari nawajibika
Uandishi sasa dini, naamini nitafika

Unaeza penda kusoma: "Kuwa Nawe ni Ajali"