Moyo wangu waugua, nasononeka kwa ndani
Nguvu zinanipungua, yaniishia imani
Laiti ningali jua, kiburi changu kiini
Nayo nishaichemua, mbelezo narudi chini
Tangu ulipoondoka, ni kweli kimeniramba
Mwenzio nahangaika, jinsi gani nitatamba
Si siri ulinichoka, wadhani yangu ya mamba
Tena yawezachipuka, kailegezeyo kamba
Nondolee hili shaka, kabisa yamenibamba
Yananichoma machozi, najizuia kulia
Kuendelea siwezi, upole najifilia
Polepole ninachizi, zanizidia hisia
Kiburi changu pwaguzi, uchungu najililia