Amuka wenzangu, Sauti yaita
Yasije machungu, zuia utata
Umuombe Mungu, kwema kujikita
Na ndipo mkoko, waalika ua
Ninawausia, kesho si ahadi
Kifo chanukia, twafata wa jadi
Ndio yetu njia, hatuna zaidi
Na ndipo mkoko, waalika ua
Kuomba ni mwiko, baba alisema
Lipo tuliziko, pata chako chema
Upate maeko, kwa njema heshima
Na ndipo mkoko, waalika ua
Fanya kwa kusudi, kujiendeleza
Huja kwa juhudi, sio kujibeza
Ibishapo hodi, umeshajikweza
Na ndipo mkoko, waalika ua