Kwaheri ya Kuonana

by JackSwaleh , August 15, 2024

Najawa na wasiwasi, sina kamwe utulivu
Moyo wapiga kwa kasi, zapungua zangu nguvu
Navunjika kwa wepesi, nakubali mi potovu
Taabu zinenikisi, nakaribia majivu

Mbona mie nasulubu, na jihisi takataka
Kuishi sina sababu, msukumo wanitoka
Njia zote masaibu, kesho sina uhakika
Kujikaza najaribu, kila muda naanguka

Pa kujificha mi sina, sina cha kunisitiri
Hali hii yanibana, rahisi nilifikiri
Yaniumiza ndoana, natazamia kaburi
Kwaheri ya kuonana, nafa na ya kwangu siri

Unaeza penda kusoma: "Kuwa Nawe ni Ajali"