Ipo siku naamini, ya kwangu yatabadili
Yatanitoka moyoni, iwe bora tena hali
Utulivu akilini, isizame yangu meli
Nikapate tu amani, dua langu kwa Jalali
Ipo siku ndugu yangu, utatabasamu tena
Yataisha tu machungu, shida itabaki dhana
Atajaza lako jungu, lolote lawezekana
Simchoke huyu Mungu, muamini utapona
Ipo siku ya baraka, tena tele kwetu sisi
Kuingo ja sitachoka, kwetu yatawa mepesi
Ipo siku itafika, yaja haraka kwa kasi
Usichoke kudamka, ye Mungu si adinasi