Angalau Rudi Baba

by JackSwaleh , August 15, 2024

Angalau rudi baba, tusemezane kwaheri
Mchungu sana hu mwiba, hadi naumwa sadiri
Tumepatwa na msiba, ni nani katusihiri
Simanzi limetukaba, kifo kimekusairi

Sote tumekuwa bubu, sauti zimetutoka
Hii nayo ni sulubu, chozi limetukauka
Nani atawa tibabu, nani atatukumbuka
Mbona wewe tu swahibu, wamenirobu hakika

Twakupa kwa pamoja, mkono wa buriani
Itafika siku moja, kupatana naamini
Unilaki kwa pambaja, nina hamu ewe kini
Sichoki mie kungoja, la isiwe tafrani

Unaeza penda kusoma: "Lawamu Za Sababu"